Mwanzo > Habari > Content

Mkataba wa ushirikiano kati ya BFSU na Chuo Kikuu cha Makhtumkuli wajumuishwa katika orodha ya mafanikio ya ziara ya Rais wa Turkmenistan

Updated: 2023-01-14

Kuanzia tarehe 5 hadi 6 Januari, 2023, Rais wa Turkmenistan Serdar Berdimuhamedov amefanya ziara nchini China kwa mwaliko wa Rais wa China Xi Jinping. Mkataba wa ushirikiano kati ya BFSU na Chuo Kikuu cha Makhtumkuli umejumuishwa katika orodha ya mafanikio ya ziara ya Rais wa Turkmenistan nchini China.

Januari 6, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Makhtumkuli cha Turkmenistan Bw. B.M.Orazdurdeyeva wametia saini mkataba wa ushirikiano kati ya vyuo vikuu viwili. Tarehe 6 Januari imesadifiana na maadhimisho ya miaka 31 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Turuimenistani, na pia ni ziara ya kwanza ya Rais Berdimuhamedov nchini China baada ya kuingia madarakani Machi 2022.

Hadi sasa, BFSU ndiyo chuo kikuu pekee nchini China kinachofundisha lugha ya Kiturkmen. Mnamo Septemba 2018, BFSU iliwaandikisha wanafunzi wa lugha ya Kiturkmen kwa mara ya kwanza. Mnamo Juni 2022, baada ya kuhitimu wanafunzi hao walianza kuhudumu katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na diplomasia ya China na Turkmenistan, uchumi, biashara na mawasiliano ya utamaduni.