Tarehe 12 Januari, Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya China (CASS) imetoa "Ripoti ya Tathmini ya AMI ya Majarida ya Sayansi ya Jamii ya China (2022)" na kutangaza matokeo ya tathmini ya mwaka 2022. Majarida 34 ya kitaaluma ya BFSU yameingia katika orodha hiyo.
Tathmini ya majarida ya sayansi ya jamii ya China imefanywa na Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya China (CASS) kila baada ya miaka minne tangu 2014. Ripoti iliyotolewa mwaka huu (2022) ni toleo la tatu. "Ripoti ya Tathmini ya AMI" ni mojawapo ya katalogi muhimu ya majarida na ina ushawishi mkubwa katika taasisi mbalimbali za utafiti.