Mwanzo > Habari > Content

Walimu wa Lugha Tano wa BFSU Watoa Huduma ya Tafsiri kwa Mkutano wa Elimu ya Kidijitali wa Dunia

Updated: 2023-02-22

Kuanzia Februari 13 hadi 14, Mkutano wa Elimu ya Kidijitali wa Dunia umefanyika mjiniBeijing. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na Mkuu wa Kitivo cha Elimu ya Mtandaoni Bi. Tang Jinlan wamehudhuria mkutano huo, walimu kutoka vitivo mbalimbali vya BFSU wamefanya kazi nzuri za ukalimani na tafsiri kwa mkutano na vikao sambamba.

Kauli mbiu ya Mkutano wa Elimu ya Kidijitali wa mwaka huu ni "Mabadiliko ya Kidijitali na Mustakabali wa Elimu", na wawakilishi kutoka zaidi ya nchi na maeneo 130 wameshiriki katika mkutano huo. Naibu Waziri Mkuu wa China Bi. Sun Chunlan ametoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano, na viongozi wengine kutoka New Zealand, Ufilipino, Uswizi na UNESCO wametoa hotuba kwa njia ya video.

Walimu hodari kutoka BFSU wamesifika kwa uwezo mkubwa wa kutafsiri, na wamechangia pakubwa kwa kufanikiwa kwa mkutano huo.