Mwanzo > Habari > Content

Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Asia ya Hangzhou Yatembelea BFSU

Updated: 2023-03-08

Tarehe 1 Machi, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Asia ya Hangzhou Bw. Xu Jianfeng amekitembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU). Makamu mkuu wa BFSU Prof. Jia Dezhong amekutana na Bw. Xu Jianfeng na wageni wengine. Pande hizo mbili zimefanya mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu huduma ya kutafsiri kwa lugha nyingi katika Michezo ya Asia ya Hangzhou.

Pande hizo mbili zimejadiliana kwa kina juu ya hali ya uendeshaji wa kituo cha huduma za lugha za kigeni, uandikishaji wa watu wanaojitolea kwa Michezo ya Asia, na upatikanaji wa huduma kwa wanaojitolea.

Baada ya mkutano, Bw. Xu Jianfeng na msafara wake wametembelea Kituo cha Huduma za Lugha za Kigeni cha Beijing na Jumba la Makumbusho ya Lugha za Dunia la BFSU.