Kuanzia tarehe 19 hadi 21 May, Kongamano la Kiswahili la 35 lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Bayreuth limefanyika katika Bayreuth. Mada ya kongamano hilo ni “ ‘Mashujaa’ na Jitihada za Kufinyanga Upya Taaluma za Kiswahili”. Zaidi ya wasomi na wataalamu 50 wanaotoka nchi mbalimbali wameshiriki katika kongamano hilo.
Mwanafunzi wa shahada ya uzamili wa BFSU Bw. Ding Ruilin ameshiriki katika kongamano hilo akiwasilisha ripoti inayohusu mchango wa mwandishi maarufu wa Tanzania Marehemu Ben Mtobwa katika maendeleo ya fasihi pendwa ya Kiswahili.
Kongamano hilo limeongeza mawasiliano kati ya Idara ya Kiswahili ya BFSU na Taaluma za Kiswahili za Kimataifa.