HOME > Habari > Content

Wang Dinghua Atembelea Ubelgiji, Hungaria na Uhispania

Updated: 2023-07-01

Kuanzia Mei 21 hadi 30, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua ameongoza ujumbe kutembelea Ubelgiji, Hungaria na Uhispania. Wametembelea vyuo vikuu, shule, Taasisi za Confucius na mashirika mbalimbali vya nchi tatu wakijadiliana juu ya miradi ya kushirikiana na kutilia saini mikataba ya kupokeana wanafunzi. Wametembelea balozi za China nchini Ubelgiji, Hungaria na Uhispania na wajumbe wa China kwenye Umoja wa Ulaya wakafanya mazungumzo na wanadiplomasia juu ya shughuli mbalimbali. Pia wamewatembelea wakurugenzi, walimu na walimu wanaojitolea wa BFSU katika Taasisi za Confucius nchini Ubelgiji, Hungaria na Uhispania.