HOME > Habari > Content

Yang Dan Atembelea Ufaransa, Uingereza na Uswisi

Updated: 2023-07-01

Kuanzia tarehe 6 hadi 15 Juni, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan ameongoza ujumbe kutembelea vyuo vikuu na taasisi mbalimbali nchini Ufaransa, Uingereza na Uswisi. Wamejadiliana juu ya ushirikiano wa nyanja mbalimbali kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na vyuo vikuu hivyo. Wametembelea ubalozi wa China nchini Ufaransa, ubalozi wa China nchini Uingereza na Ujumbe wa Kudumu wa China kwenye Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), na kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa ubalozini. Pia wamewatembelea baadhi ya wahitimu, wanafunzi na walimu wa BFSU walioko nchini Ufaransa, Uingereza na Uswisi.