HOME > Habari > Content

Sherehe ya Kuwasindikiza Wanafunzi Wanaotarajali katika Nje ya Nchi Yafanyika BFSU

Updated: 2023-07-21

Mnamo tarehe 30 Juni, BFSU imefanya sherehe ya kuwasindikiza wanafunzi wanaotarajali katika nje ya nchi. Wageni wanaotoka mashirika mbalimbali yakiwemo Benki Kuu ya China, Wizara ya Elimu na kadhalika wamehudhuria sherehe hiyo.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan ametoa hotuba yenye mada ya “Kutekeleza majukumu ya ulimwengu na kuonyesha taswira ya China”. Pia, walimu wengine wanaoongoza timu wametoa hotuba.

Prof. Yang Dan ametangaza kuwa timu za kutarajali kwa wanafunzi katika nje ya nchi zitafunga safari rasmi, na wageni wameikabdhi bendera kwa walimu wanaoongoza timu 43.

Programu hii yenye kaulimbiu ya Ustaarabu wa Kimataifa na Wajibu wa Vijana ni ya kwanza ya kutarajali katika nje ya nchi ambayo inawawezasha wanafunzi kufanya kazi au utafiti katika nje ya nchi. Mwaka huu, BFSU itatuma jumla ya timu 43 zitakazojumuisha zaidi ya walimu na wanafunzi 500 kutarajali katika nchi mbalimbali.