Mnamo tarehe 23 Mei, “Jukwaa la Maendeleo ya Tibet ya China la 2023” limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Beijing. Kaulimbiu ya jukwaa hilo ni "Zama Mpya, Tibet Mpya na Safari Mpya". Jukwaa hilo limeandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, Serikali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet pamoja na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing.Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang...
Mnamo tarehe 4 Mei, Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini China Bw. Ali Obaid Al Dhaheri ametembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amekutana na Bw. Dhaheri na msafara wake. Wamejadiliana juu ya kuimarisha ushirikiano katika kupelekeana wanafunzi, mafunzo ya pamoja na mawasiliano ya kitaaluma. Baada ya mkutano, Bw. Dhaheri ...
Kuanzia tarehe 16 hadi 23 Aprili, Makamu Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian ameongoza ujumbe kutembelea Jamhuri ya Czech na Jamhuri ya Italia. Wametembelea vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo Chuo Kikuu cha Palacký, Chuo Kikuu cha Roma cha Italia, Chuo Kikuu cha Mashariki cha Naples na kadhalika ili kuimarisha ushirikiano wa nyanja mbalimbali kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na vyuo vi...
Tarehe 9 Aprili, "Kamusi ya Sayansi ya Jamii ya Kichina-Kitibet-Kiingereza" imetolewa katika Taasisi ya Utafiti wa Tibet ya China mjini Beijing. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing pamoja na Shirika la Uchapishaji la Biashara.Kamusi ya Sayansi ya Jamii ya Kichina-Kitibet-Kiingereza ni matunda ya mradi mkubwa wa kimsingi wa utafiti wa sayansi ya jamii wa Tibet a...
Tarehe 3 Aprili, Mkurugenzi wa Ofisi ya Asia Mashariki ya Shirika la Msalaba Mwekundu Bw. Pierre Krähenbühl ametembelea BFSU. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amekutana na Bw. Pierre Krähenbühl na ujumbe wake.Pande hizo mbili zimejadiliana juu ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali zinazowahusisha wanafunzi zikiwemo kupata ajira, kutoa huduma ya kujitolea na mawasiliano ya kitaaluma....
Tarehe 31 Machi, Rais wa Chuo Kikuu cha Queensland cha Australia Bi. Deborah Terry ameongoza ujumbe kutembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amekutana na Bi. Deborah Terry na msafara wake. Pande hizo mbili zimetiliana saini "Mkataba wa Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na Chuo Kikuu cha Queensland".
Tarehe 23 Machi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Belarusi Bw. Andrei Karol ameongoza ujumbe kutembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amezungumza na Bw. Andrei Karol, na vyuo vikuu viwili vimetilia saini mkataba wa kupelekeana wanafunzi.
Tarehe 20 Machi, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kifaransa yamefanyika kwenye Ubalozi wa Ufaransa nchini China. Wizara ya Elimu ya Ufaransa imemtunukia Mkuu wa Kitivo cha Kifaransa cha BFSU Prof. Dai Dongmei tuzo ya Academic Palm Knight kwa kuzingatia mchango wake katika kuendeleza elimu ya Kifaransa na kueneza utamaduni wa Kifaransa. Balozi mpya wa Ufaransa nchini China Bw. Bertra...
Tarehe 20 Machi, Balozi wa Kazakhstan nchini China Bw. Shakhrat Nuryshev ametembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya kwanza ya kitaifa ya lugha ya Kikazakh. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amekutana na Bw. Shakhrat Nuryshev na msafara wake. Wamefanya mazungumzo ya kina kuhusu ushirikiano wa kutoa mafunzo ya tafsiri na ukal...
Tarehe 20 Machi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Western Sydney cha Australia Bw. Barney Glover ametembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing.Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amekutana na Bw. Barney Glover na msafara wake. Wamejadiliana juu ya mawasiliano ya wanafunzi na walimu wa pande mbili, mafunzo ya pamoja, programu za shahada ya uzamili na kadhalika.
Tarehe 18 Machi, Kongamano la Ujenzi wa Rasilimali za Taarifa za Taaluma ya Nchi na Maeneo lililoandaliwa na Jumuiya ya Utafiti wa Taaluma ya Nchi na Maeneo limefanyika katika Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amehudhuria kongamano hilo.Wataalamu na wasomi 96 wanaoshughulikia Utafiti wa Taaluma ya Nchi na Maeneo kutoka vyuo vikuu 34 wameshiri...
Tarehe 1 Machi, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Asia ya Hangzhou Bw. Xu Jianfeng amekitembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU). Makamu mkuu wa BFSU Prof. Jia Dezhong amekutana na Bw. Xu Jianfeng na wageni wengine. Pande hizo mbili zimefanya mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu huduma ya kutafsiri kwa lugha nyingi katika Mich...
Tarehe 24 Februari, vitabu vipya vya "Mradi wa Kutafsiriana Maandishi Maarufu ya Nchi za Asia" vimetolewa katika ufunguzi wa Mkutano wa 35 wa Maagizo ya Vitabu uliofanyika kwenye Kituo cha Maonyesho cha Kimataifa mjini Beijing.Miongoni mwa Vitabu hivi, The Life and Revolutionary Cause of Chairman Kaysone Phomvihane, The Two Sisters na The Legend of Khun Borom vilitafsiriwa na walimu wa Kilaos w...
Kuanzia Februari 13 hadi 14, Mkutano wa Elimu ya Kidijitali wa Dunia umefanyika mjiniBeijing. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na Mkuu wa Kitivo cha Elimu ya Mtandaoni Bi. Tang Jinlan wamehudhuria mkutano huo, walimu kutoka vitivo mbalimbali vya BFSU wamefanya kazi nzuri za ukalimani na tafsiri kwa mkutano na vikao sambamba.Kauli mbiu ya Mkutano wa Elimu ya Kidijitali wa mwaka huu ni ...
Tarehe 12 Januari, Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya China (CASS) imetoa "Ripoti ya Tathmini ya AMI ya Majarida ya Sayansi ya Jamii ya China (2022)" na kutangaza matokeo ya tathmini ya mwaka 2022. Majarida 34 ya kitaaluma ya BFSU yameingia katika orodha hiyo. Tathmini ya majarida ya sayansi ya jamii ya China imefanywa na Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya China (CASS) kila baada ya miaka minne tangu 2...
Kuanzia tarehe 5 hadi 6 Januari, 2023, Rais wa Turkmenistan Serdar Berdimuhamedov amefanya ziara nchini China kwa mwaliko wa Rais wa China Xi Jinping. Mkataba wa ushirikiano kati ya BFSU na Chuo Kikuu cha Makhtumkuli umejumuishwa katika orodha ya mafanikio ya ziara ya Rais wa Turkmenistan nchini China.Januari 6, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Makhtumkuli ...
Tarehe 18 Desemba, Kongamano la Jumuiya ya Taaluma ya Nchi na Maeneo ya Kimataifa la 2022(CCAS) lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing limefanyika kwenye mtandao. Kaulimbiu ya kongamano hilo ni “Ujumuishi, Ushirikiano na Maendeleo Endelevu ya Ulimwengu".Jumuiya ya Taaluma ya Nchi na Maeneo ya Kimataifa (CCAS) ni mtandao wa kitaaluma ulioanzishwa na Shirikisho la Kimataifa...