HOME > Kuhusu BFSU > Mandhari ya Chuo > Content

Maktaba

Updated: 2021-07-12

Maktaba ya BFSU inahifadhi vitabu vipatavyo milioni 1.57 na vitabu pepe milioni 2.16, magazeti na majarida 1,081, majarida pepe elfu 38 na database 107 hasa katika vipengele vya lugha, fasihi na utamaduni. Sambamba na ukuaji wa mitalaa mtambuko, machapisho ya sheria, diplomasia, uchumi, uandishi wa habari na usimamizi yamekusanywa kibao miaka ya karibuni.

Maktaba ya BFSU ina ghorofa sita na jumla ya eneo lake ni mita za mraba elfu 23 hivi. Licha ya nafasi za kujisomea zaidi ya 2,200 na vyumba vya kusomea 18, maktaba pia inatoa vyumba vya mikutano, vyumba vya mihadhara, ukumbi wa maonesho na mgahawa ambavyo vinawapatia walimu na wanafunzi nafasi za kuzungumza na kubadilishana mawazo.

Maktaba imeweka mashine ya kurudishia vitabu masaa 24 pamoja na huduma nyingine kama kuchapa, kunakili, kuskani n.k. Matumizi ya vifaa vya multimedia na teknolojia ya kisasa yanasaidia sana kuboresha usimamizi na huduma yetu.

Yote hayo ya hazina kubwa, mazingira murua, huduma bora na vifaa vya kisasa yameipelekea maktaba yetu iwe mahala pa kuvutia walimu na wanafunzi kusoma, kutafiti na kuwasiliana baina yao humu ndani.