HOME > Habari > Content

Kamishna wa EU Atembelea BFSU

Updated: 2024-04-14

Tarehe 30 Machi, Kamishna wa Kamati ya Ubunifu, Utafiti, Utamaduni, Elimu na Shughuli za Vijana ya Umoja wa Ulaya (EU) Bi. Iliana Ivanova ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Naibu Waziri wa Elimu Bw. Chen Jie, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Mawasiliano ya Kimataifa Bw. Yang Dan, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian wamejitokeza kumkaribisha.

Bw. Chen Jie amewazawadia Kamishna Bi. Ivanova, Mjumbe wa EU nchini China Bw. Tuo Yaohui na Mkuu wa Idara ya Elimu na Utamaduni wa EU Bi. Pia Ahrenkilde Hansen vitabu vilivyohaririwa, kutafsiriwa na kuchapishwa na BFSU vikiwemo Ndoto ya Nyumba Nyekundu cha Kibulgaria, Kitabu cha Utamaduni wa China cha Kihispania na Mazungumzo ya Kidanish. Prof. Wang Dinghua na Kamishna Bi. Ivanova wametoa hotuba.

Baada ya sherehe, wageni hawa wamekwenda Idara ya Kibulgaria ya Kitivo cha Lugha na Utamaduni wa Ulaya cha BFSU na kuzungumzia hali ya Kibulgaria na kozi nyingine za lugha za EU. Pia wametembelea Bustani ya Urafiki wa China na Ulaya iliyojengwa mwaka 2015.