HOME > Habari > Content

Ujumbe wa BFSU Watembelea Nepal, Vietnam na Indonesia

Updated: 2024-04-28

Kuanzia tarehe 8 hadi 17 Aprili, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua ameongoza ujumbe wa chuo kutembelea Nepal, Vietnam na Indonesia. Wametembelea Chuo Kikuu cha Tribhuvan, Chuo Kikuu cha Kathmandu, Chuo Kikuu cha Sanskrit cha Nepal (Kathmandu), Chuo Kikuu cha Sheria cha Hanoi, Chuo Kikuu cha Biashara ya Nje cha Vietnam, Chuo Kikuu cha Sheria cha Hue na Chuo Kikuu cha Ualimu cha Indonesia.

Zaidi ya hayo, Prof. Wang Dinghua na wajumbe wametembelea Idara ya Maendeleo na Ujenzi wa Lugha ya Bandung iliyo chini ya Wizara ya Elimu ya Indonesia na idara nyingine za serikali. Pande hizo mbili zimekubaliana kutafuta mbinu mpya za ushirikiano wa vyuo, idara za serikali, utafiti wa nchi na maeneo, ufundishaji na mawasiliano ya walimu na wanafunzi kwa pamoja.

Pia wametembelea balozi za China katika nchi hizo tatu na ubalozi mdogo mjini Ho Chi Minh. Wamesalimiana na wahitimu wa BFSU, kutembelea makampuni ili kuwatafutia wanafunzi nafasi za ajira na kuanzisha Jumuiya ya Wahitimu wa BFSU nchini Indonesia.