HOME > Taaluma > Walimu

Kitivo cha Masomo ya Afrika

Updated: 2021-08-20

非洲学院(1).jpg

Kiswahili kinatumiwa katika eneo kubwa la Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda na nchi nyingine majirani. Inakadiriwa kuwa watu wapatao milioni 150 wanatumia lugha hiyo. Mwaka 2021, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetangaza tarehe 7 Julai kuwa Siku ya Kiswahili Duniani.

BFSU imeanzisha kozi ya Kiswahili tangu mwaka 1961 ambayo ni lugha ya kwanza ya Afrika inayosomeshwa hapa. Katika miongo kadhaa iliyopita, kozi hiyo imetayarisha wasomi wa Kiswahili zaidi ya 230. Hivi sasa kozi hiyo ina walimu wawili wa China na maprofesa wawili wa Afrika. Mwaka 2022, kozi hiyo imeorodheshwa katika kozi za daraja la juu na Wizara ya Elimu ya China.

Kozi hiyo inaandikisha wanafunzi wa shahada ya kwanza kila baada ya miaka minne. Wanafunzi wanasomeshwa matamshi, sarufi, mazungumzo, usikilizaji, tafsiri, ukalimani, uandishi, taarifa za habari, fasihi, utamaduni wa Kiswahili n.k. Katika mwaka wa tatu wanafunzi wana fursa ya kusoma katika nchi za Afrika kwa miezi 6-12. Hivi sasa tumeanzisha ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Nairobi na Chuo Kikuu cha Kenyatta. Aidha, kozi yetu inaandikisha wanafunzi wa shahada ya uzamili kila mwaka.

Licha ya Kiswahili, wanafunzi pia wanaweza kujifunza masomo ya Kiingereza, siasa, uchumi, diplomasia, sheria, fedha, biashara, uhasibu, usimamizi na mengineyo. Pia wanaweza kushiriki mtihani wa Kiingereza wa ngazi ya kitaifa na ufaulu wao unafikia 70%.

Sifa na umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili umekubaliwa na idara mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Wahitimu wetu wanapata ajira katika Wizara ya Mambo ya Nje, mashirika ya umma, makampuni ya kimataifa, vyombo vya habari vya kitaifa, vyuo vikuu na taasisi. Pia wapo wengi wamepokewa na vyuo vikuu maarufu vya Ulaya na Marekani kuendelea na masomo yao ya shahada ya uzamili.