HOME > Habari > Content

Mkuu wa SOAS Atembelea BFSU

Updated: 2024-03-16

Tarehe 12 Machi, Mkuu wa SOAS Bw. Adam Mohamed Habib na msafara wake wametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Jia Wenjian wamekutana na wageni hawa.

Prof. Wang Dinghua ameeleza habari za maendeleo ya taaluma na mawasiliano ya kimataifa ya BFSU, na ametumai kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili katika kuendeleza masomo, kuandalia wanafunzi na kufanya utafiti kwa pamoja.

Bw. Habib ameeleza habari za SOAS, pia ametumai kuimarisha ushirikiano wa mafunzo na utafiti kwa pande zote, na kutafuta njia mpya za kuandalia na kuendeleza vijana pamoja na BFSU.

Pande hizo mbili zimetia saini mkataba wa ushirikiano wa wanafunzi wa shahada ya uzamili.