HOME > Habari > Content

BFSU Yapanga Kazi za Muhula wa Spring wa 2024

Updated: 2024-03-06

Mnamo tarehe 28 Februari, kikao cha kufungua muhula wa Spring wa 2024 kimefanyika BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amepanga kazi za muhula huu kwa pande zote.

Prof. Wang Dinghua ameweka wazi mambo kumi ya kufanya. Kwanza, kutathmini na kukuza elimu ya shahada ya kwanza kwa vigezo vizuri. Pili, kupanga mikakati ya maendeleo ya taaluma. Tatu, kuharakisha ujenzi wa “Chuo na Taaluma Bora Duniani”. Nne, kuimarisha ujenzi wa Chama na siasa kwa pamoja. Tano, kuandalia wanafunzi kwa pande zote. Sita, kutayarisha kundi la makada bora. Saba, kurahisisha muundo wa idara. Nane, kuboresha usimamizi wa Chuo. Tisa, kuzidisha mawasiliano ya kimataifa. Kumi, kuhakikisha huduma za kimsingi.