CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kituo cha Utafiti wa Elimu ya Lugha za Kigeni cha China

Kituo cha Utafiti wa Elimu ya Lugha za Kigeni kilichoanzishwa mwaka 2000 kimeidhinishwa na Wizara ya Elimu kama ni mojawapo ya Taasisi muhimu za Utafiti wa Sanaa na Sayansi ya Jamii.

Kituo hiki kinachunguza masuala mawili hasa ambayo ni: (i) Elimu ya Lugha za Kigeni; (ii) Isimu na Isimu Linganishi. Na tafiti zake zinalenga zaidi ufundishaji, ujifunzaji na tathimini ya lugha za kigeni. Majukumu yake makuu ni kama yafuatayo: 1) Kufanya miradi ya utafiti na kujijenga kituo muhimu cha utafiti chenye hadhi ya kitaifa 2) Kuwatayarisha watafiti wenye ubunifu wa hali ya juu c) Kujenga kituo cha rasilimali na taarifa za elimu ya lugha za kigeni na kukuza mawasiliano ya kitaaluma d) Kutoa ushauri kuhusu mageuzi na maendeleo ya elimu ya lugha za kigeni nchini China.

Hadi sasa, kituo hiki kina watafiti wapatao 13 wakiwemo watafiti 10 na watafiti washiriki 2 ambao wote wamepata shahada ya uzamivu. Kituo hiki kimezaa matokeo maridhawa ya utafiti. Kati ya mwaka 2009 hadi 2015, kituo hiki kimekabidhiwa miradi 46 ya utafiti na kimechapisha vitabu na makala 430. Tena kimepata tuzo mara nyingi. Kama ni kituo muhimu cha kuwafunza wataalamu wa lugha za kigeni, kituo hiki pia kinawasajili wanafunzi 20 wa shahada ya uzamili na wanafunzi 20 wa shahada ya uzamivu kila mwaka. Hivi sasa kuna watu 5 wanaofanya utafiti baada ya kupata shahada ya uzamivu kituoni mwetu.

Hivi karibuni kituo hiki kimezindua asasi tatu mpya:

Skuli ya Elimu

Skuli ya Elimu ilianzishwa tarehe 17 Juni 2015 ili kukuza mitalaa ya elimu, kuinua kiwango cha utafiti na kuwafunza walimu wenye sifa wa lugha za kigeni.

Skuli hii ina maprofesa wanne ambao wote ni washauri wa wanafunzi wa Ph.D na profesa mmoja mshiriki. Shule hii inafanya tafiti zake katika maeneo matatu ambayo ni: Kozi za Lugha na Ufundishaji; Mafunzo ya Walimu wa Lugha na Elimu Linganishi na Elimu ya Kimataifa.

Skuli hii imepiga hatua kubwa katika mafunzo ya ualimu. Kwa mfano, imeandaa mafunzo ya walimu vijana wa vyuo vikuu kwa miaka 10 mfululizo na imetoa mafunzo ya walimu wa Kiingereza wa shule za sekondari na za msingi jijini Beijing. Katika siku za mbele tutaandaa mafunzo kwa walimu wapya kabla ya kuingia kazini.

Kituo cha Tathimini ya Lugha za Kigeni cha China

Kituo hiki kilizinduliwa mnamo tarehe 29, Septemba, 2014 kikilenga kujijenga kama taasisi ya upimaji wa lugha za kigeni yenye ushawishi nchini China. Kituo hiki kinajishughulisha na uandaaji wa majaribio ya lugha za kigeni, kusanifisha kigezo cha upimaji wa lugha za kigeni na kuandaa majaribio maalum kwa ajili ya watahiniwa mahususi. Ni matumaini yetu kwamba kituo hiki kitaweza kutoa huduma za upimaji wa lugha za kila aina ili kukidhi mahitaji ya ngazi zote.

Kituo cha Utafiti wa Ukuaji wa Lugha cha Taifa

Kituo hiki kilianzishwa Julai 2014 na kiko chini ya usimamizi wa Idara ya Lugha ya Wizara ya Elimu na BFSU. Dhima kuu ya kituo hiki ni kuchunguza nafasi ya lugha katika siasa na diplomasia ya taifa, kuchunguza nadharia na maendeleo ya uwezo wa lugha ya China, kutafiti rasilimali watu za lugha nchini China, sera ya lugha ya mataifa makubwa na uwezo wa matumizi ya lugha za kigeni katika majiji makubwa ili kutoa mapendekezo kwa mamlaka husika na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC