CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Kiingereza

Kitivo cha Kiingereza kina idara ya Kiingereza na idara ya Tafsiri na Ukalimani ambazo zimeweka programu za Ph.D za Lugha na Fasihi ya Kiingereza na Mtalaa wa Tafsiri na Ukalimani. Siku zote kitivo hiki kinaboresha mbinu za ufundishaji na mfumo wa masomo wa kuunganisha lugha na maarifa ili kuwatayarisha wasomi wenye sifa na kujenga kitivo kitakachojulikana duniani.

Hadi sasa kitivo kina walimu 96 wakiwemo maprofesa 27, maprofesa washiriki 28 na kati yao walimu 66 wamepata shahada ya uzamivu. Kuna wanafunzi 599 wa shahada ya kwanza, wanafunzi 381 wa shahada ya uzamili na wanafunzi 87 wa shahada ya uzamivu ambao wana ustadi mkubwa wa lugha na tafsiri, maarifa mapana na uwezo wa uchunguzi na ubunifu.

Kitivo cha Kiingereza kinashirikiana vizuri na vyuo vikuu 30 vya Uingereza, Marekani, Australia, Kanada, New Zealand kama vile Lancaster, Columbia, Adelaide, Toronto, Auckland n.k. Mbali na kuwapeleka wanafunzi, kitivo pia kinawapokea wanafunzi wa nje kusoma kwetu.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1944, kitivo hiki kimetayarisha maelfu ya mahiri wanaobobea katika sekta za diplomasia, biashara, fedha, vyombo vya habari, elimu, ukalimani na nyinginezo. Baadhi ya wahitimu mashuhuri ni pamoja na: Li Zhaoxing, Sun Zhenyu, Zhang Yesui, Fu Ying, Jin Liqun, Zhang Qiyue, Yang Lan, Xu Gehui, Sun Ning. Hivi leo, wanafunzi hupata ajira katika wizara, mashirika ya umma na ya kimataifa, vyombo vya habari, vitengo vya mambo ya nje, taasisi za elimu na utamaduni, tasnia za uchapishaji n.k. Pamoja na hayo, zaidi ya 30% ya wanafunzi wanajiunga na Chuo Kikuu cha Oxford, Chuo Kikuu cha Harvard na vinginevyo maarufu ili kujiendeleza kitaaluma.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC