CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Taasisi ya Sanaa

Taasisi ya Sanaa iliasisiwa mwaka 2011 kwa madhumuni ya kukuza na kusambaza sanaa za kijadi za China. Jukumu lake kubwa ni kuwaelewesha walimu na wanafunzi wa BFSU, wanafunzi wageni, wafanyakazi wa vitengo vya mambo ya nje na taasisi za confucius nadharia na utendaji wa sanaa za kijadi hasa maigizo ya Beijing.

Hivi sasa kuna wanafunzi 9 wa shahada ya uzamili wanaosoma usambazaji wa maigizo ya kijadi. Masomo yaliyopo kwa sasa ni kama yafuatayo: Mawasiliano ya Sanaa, Historia ya Tamthiliya ya China na Nje, Historia ya Filamu ya China na Nje, Mantiki ya Sanaa (Aesthetics), Utangulizi wa Sanaa, Nadharia ya Sanaa ya Magharibi, Uigizaji na Uongozaji wa Kimsingi n.k.

Taasisi ya Sanaa inautilia maanani ufundishaji wa nadharia na vitendo. Mbali na masomo ya darasani, wanafunzi pia wamejituma katika mradi wa “Tafsiri ya Kiingereza ya Maigizo 100 ya Beijing” ili wazidishe uelewa juu ya sanaa ya maonesho ya kijadi.

Taasisi hii ina walimu 4 na wataalamu wa nje 12 wakiwemo maprofesa 6, maprofesa washiriki 2 na walimu wazamivu 8.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC