CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Masomo ya Asia-Afrika

Kitivo cha Masomo ya Asia-Afrika kiliasisiwa mwaka 1961 na ni taasisi yenye historia ndefu na idadi kubwa ya lugha kuliko zote nchini. Mpaka sasa lugha 33 za Asia na Afrika zinafundishwa kwenye kitivo hiki. Kuna vituo kadhaa vya utafiti wa kanda na nchi ikiwa ni pamoja na Asia ya Kusini-Mashariki, Asia ya Kusini, Asia ya Magharibi na Afrika, Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini, Sri Lanka, Indonesia na Iran. Kila mwaka matunda kemkem ya utafiti yanachapishwa kwenye jarida la “Asian and African Studies”.

Kitivo cha Masomo ya Asia-Afrika kina walimu 50 wakiwemo maprofesa 7, maprofesa washiriki 13 na walimu wazamivu 21. Aidha, kitivo hiki kinawaalika wataalamu kutoka nchi zaidi ya 10 na wasomi mashuhuri wa nchini wakishiriki katika kazi za ufundishaji. Hivi sasa idadi ya wanafunzi wa ngazi zote imefikia 500. Mbali na masomo ya lugha, wanafunzi wanapewa elimu ya mitalaa ya kila aina hususan masomo ya utafiti wa kanda. Katika nusu karne iliyopita, maelfu ya wanafunzi wenye umahiri mkubwa wa lugha, mtazamo mpana wa ujuzi na tabia na maadili mema walihitimu kutoka kitivo hiki.

Katika miaka michache ijayo, kitivo hiki kinatarajiwa kuwa na raslimali za kutosha za ufundishaji na utafiti; kitakamilisha masomo ya ngazi zote za shahada ya awali, uzamili na uzamivu; kitakuwa kitovu cha msingi cha kuwaandaa wanafunzi wenye umahiri wa lugha na sifa bora ya kimataifa; kitakuwa kitovu muhimu cha utafiti wa kanda ya Asia na Afrika kikiendana na mikakati ya taifa na mahitaji ya jamii.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC