CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Elimu ya Mtandao na Elimu ya Watu Wazima

发布时间:2019-04-28

Kitivo cha Elimu ya Mtandao na Elimu ya Watu Wazima kiliasisiwa mwaka 2013 kutokana na muungano wa vitengo vinne vya watu wazima, mafunzo, elimu ya mtandao na mafunzo ya Tongwen. Hivi sasa kuna walimu na wafanyakazi 115 wakiwemo wa kudumu na wa muda.

Kitivo hiki kinatoa elimu za cheti na digrii kwa pamoja ambazo ni nyongeza muhimu ya huduma za jamii za BFSU. Katika kitivo hiki kuna mafunzo ya maandalizi kwa wanafunzi wanaodhaminiwa na serikali na kituo cha mitihani cha Wizara ya Elimu. Programu ya elimu ya watu wazima inawasajili wanafunzi 200 kila mwaka na wahitimu wetu wanasifika kwa umahiri wao wa hali ya juu. Elimu ya Mtandao ikitumia teknolojia ya kisasa imeweka masomo saba ya Kiingereza, Uongozi wa Biashara, Uhasibu, Fedha, Biashara ya Mtandao, Menejimenti ya Mfumo wa Habari, Biashara ya Kimataifa na wanafunzi wanaosajiliwa wamefikia 45,000. Aidha, kitivo hiki kimeshirikiana na Wizara ya Usalama wa Raia, Mamlaka ya Hali ya Hewa, Benki ya China, Benki ya Ujenzi ya China, Kampuni ya Mafuta ya Petroli ya China (CNPC), Shirika la Ndege la Kusini la China n.k. katika kuwafunza wafanyakazi wao.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC