CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Idara ya Michezo

Idara ya Michezo ina majukumu yafuatayo: ufundishaji wa michezo; mafunzo ya timu za michezo; mashindano mbali mbali ya michezo; upimaji wa afya ya wanafunzi na shughuli nyingine husika.

Kuna walimu 16 wakiwemo maprofesa washiriki 9 na wahadhiri 6. Kati yao walimu 5 wamepata shahada ya uzamili.

Katika chuo chetu kuna timu 11 za michezo ikiwa ni pamoja na mpira wa kikapu wa wanaume na wanawake, mpira wa wavu wa wanaume na wanawake, mpira wa miguu wa wanaume na wanawake, mpira wa vinyoya, mpira wa tenisi, mpira wa mezani, riadha, mazoezi ya viungo na kuogelea. Timu zote zimepata mafanikio maridhawa katika michuano mbalimbali ya vyuo vikuu nchini.

Tangu mwaka 2010 chuo chetu kimeanza kusajili wanafunzi wenye kipaji cha kuogelea. Idara hii inasimamia mazoezi, masomo na mashindano ya wanafunzi hawa ikishirikiana na Kitivo cha Uhusiano wa Kimataifa.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC