CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Lugha na Utamaduni wa Ulaya

发布时间:2019-04-28

Kitivo cha Lugha na Utamaduni wa Ulaya (SELC) kilichozinduliwa mwaka 1954 kinashika hatamu hapa nchini kwa historia yake ndefu na idadi ya lugha zinazofundishwa. Mpaka sasa lugha zote rasmi 25 za Umoja wa Ulaya zimezinduliwa na kati yao lugha 15 zinafundishwa peke yetu. Licha ya Kituo cha Utafiti wa Ulaya ya Kati na Mashariki kilicho chini ya Wizara ya Elimu, zipo taasisi nyingine kadhaa zinazochunguza Finland, Poland, nchi za Ulaya ya Kaskazini n.k. Katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, kitivo hiki kimekuwa kitovu cha utafiti wa lugha na utamaduni wa Ulaya tena ni dirisha la ushirikiano wa elimu kati ya China na Ulaya.

Kitivo cha SELC kinasajili wanafunzi wa ngazi zote ambapo mnamo Septemba 2015 wanafunzi wa shahada ya kwanza ni 409 huku wasomao shahada ya pili na ya juu ni 24 na 10. Mbali na mafunzo ya lugha, wanafunzi wanapangiwa masomo mbali mbali ya utafiti wa nchi husika, Kiingereza, lugha ya tatu na mengineyo. Karibu wanafunzi wote wana fursa ya kusomea nchi za nje kwa miezi sita au mwaka mzima.

Miongoni mwa walimu 49 waliopo kwa sasa, kuna maprofesa 5 wakiwemo washauri wanne wa shahada ya uzamivu, maprofesa washiriki 13 na walimu 14 ambao wameshachukua shahada ya uzamivu. Walimu hao wametoa mchango mkubwa katika utungaji wa vitabu na kamusi, tafsiri ya fasihi, mawasiliano ya elimu n.k. huku baadhi yao wanajulikana ndani na nje ya nchi mithalani Prof. Yi Lijun, Prof. Feng Zhichen, Prof. Gong Kunyu, Prof. Wang Jun na Prof. Ding Chao. Kitivo hiki kimezindua jarida la “Ulaya ya Mashariki”, juzuu za “Uchunguzi wa Lugha na Utamaduni wa Ulaya” na “Ufundishaji na Ujifunzaji wa Lugha za Ulaya” ambazo zinachapisha makala mbali mbali za utafiti.

Kwa upande wa ushirikiano wa kimataifa, kila mwaka kitivo hiki kinapokea viongozi waandamizi kutoka nchi mbali mbali za Ulaya. Pamoja na kufundisha lugha na tamaduni za Ulaya, kitivo hiki kinapania kuieneza China katika nchi za Ulaya. Miaka ya karibuni, walimu wetu wameshiriki katika ujenzi na uendeshaji wa taasisi za Confucius katika Chuo Kikuu cha Eötvös Loránd Hungary, Krakow Poland, Chuo Kikuu cha Sofia Bulgaria, Chuo Kikuu cha Palacky Czech na Chuo Kikuu cha Rome La Sapienza Italia.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC