CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Idara ya Kompyuta

Idara ya Kompyuta ilianzishwa mwaka 2009 na asili yake ilikuwa kituo cha kompyuta kilichoanzishwa mwaka 1990.

Hadi sasa kuna walimu 11 ambao wengi wamepata shahada ya uzamivu. Miaka ya karibuni, walimu wa idara hiyo wamedhaminiwa na mifuko ya kitaifa katika programu 2 za sayansi ya maumbile, programu 2 za sayansi ya jamii na programu 6 za kimkoa. Isitoshe, walimu wamechapisha makala 26 kwenye majarida ya SCI, EI au CSSCI.

Idara hii inadhamiria kutayarisha wanafunzi ambao wanabobea katika Kiingereza, biashara na teknolojia ya kompyuta ili waende sambamba na maendeleo ya tehama na utandawazi.

Kila mwaka idara hii inadahili wanafunzi wa darasa moja na kuna wanafunzi 93 kwa sasa ambao wamepata tuzo kadha wa kadha katika mashindano ya kitaifa na kimataifa. Miongoni mwa wahitimu wa idara hiyo, theluthi moja wamekwenda kusomea nchi za nje, theluthi moja wanaendelea kusoma katika vyuo vikuu vya nchini na theluthi nyingine wamepata kazi katika benki, serikali au makampuni ya tehama.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC