CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Kimataifa

Kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Kimataifa (kwa ufupi “SIJC”) kilizinduliwa mwaka 2014 baada ya kujitenga na Kitivo cha Kiingereza. Ufupisho wake “SIJC” umejenga kauli mbiu ya kitivo: Jidhibiti (Self-discipline), Uhuru (Independence), Haki (Justice) na Ushirikiano (Cooperation).

Kitivo hiki kinadhamiria kuwajengea wanafunzi uelewa mpana wa mtalaa, ustadi mkubwa wa lugha, maadili mema na sifa bora za kufanyia kazi.

Kwa sasa kitivo hiki kina walimu 13 wakiwemo maprofesa wanne na maprofesa washiriki wawili. Walimu 12 wameshapata shahada za uzamivu. Aidha, kitivo chetu kinawaalika watalaamu wa nje wanaobobea katika fani ya vyombo vya habari waje kufundisha ama kuandaa mihadhara mbali mbali. Mkuu wa kitivo pia anatoka nchi ya nje.

Kwa sasa kitivo hiki kina wanafunzi wapatao 200 wa shahada ya kwanza na wanafunzi 60 wa shahada ya uzamili wakisoma Uandishi wa Habari au Mawasiliano ya Kimataifa. Programu ya shahada ya uzamivu yenye vipengele vinne (Mawasiliano ya Tamaduni Mbalimbali, Uandishi wa Habari wa Vyombo vyote, Mawasiliano ya Kimkakati na Mawasiliano ya Lugha Lengwa) itaanzishwa mwaka 2016.

Mbali na hayo, kitivo hiki kina taasisi nne za utafiti ambazo ni: Kituo cha Utafiti wa Uandishi wa Habari wa Kimataifa, Kituo cha Utafiti wa Mawasiliano ya Habari ya Kimataifa, Kituo cha Utafiti wa Maadili na Sera ya Habari na Taasisi ya Lugha ya Historia na Mawasiliano ya Kimkakati.

Masomo ya shahada ya awali yana nguzo tatu: Ustadi wa lugha ya Kiingereza, Uandishi wa habari na Mawasiliano na Masomo mengine husika kama diplomasia, utamaduni, siasa n.k. Wanafunzi wanapohitimu lazima wafaulu kwenye mtihani wa Kiingereza daraja la 8 (TEM 8) na kuandika tasinifu kwa Kiingereza. Asilimia 90 ya kozi zinasomeshwa kwa Kiingereza ili kuinua uwezo wa wanafunzi kuitumia lugha hiyo. Isitoshe, wanafunzi wanaweza kujifunza lugha ya pili ya kigeni na masomo mengine kama wapendavyo.

Kitivo chetu pia kinazingatia mazoezi nje ya darasa. Pamoja na kuandaa gazeti la wanafunzi107 Investigation, kitivo chetu kinawahimiza wanafunzi wafanye mazoezi kwenye vyombo vya habari mbali mbali, kama vile Shirika la Habari la Xinhua, Gazeti la China la Kila Siku (China Daily), Redio China Kimataifa (CRI), Kituo cha Televisheni cha China (CCTV) n.k.

Kwa upande wa ushirikiano wa kimataifa, kitivo chetu kinashirikiana na vyuo vikuu kadha wa kadha vya Marekani, Uiingereza, Australia, New Zealand, Ireland, Austria n.k.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC