CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Biashara ya Kimataifa

Kitivo cha Biashara ya Kimataifa kilianzishwa mwaka 2001 na programu zake zinajumuisha shahada ya kwanza, ya uzamili, ya uzamivu, ya ushirikiano wa pamoja, mafunzo ya muda n.k. Hadi sasa kuna wanafunzi zaidi ya 1, 000 na wanafunzi wageni 400 kutoka nchi 50 duniani.

Kitivo hiki kinalenga kuwa kitivo cha kiutandawazi kinachojumuisha mahiri wa biashara wenye ubunifu na upeo mpana na kuunganisha biashara kati ya China na dunia.

Katika miaka michache iliyopita, kitivo hiki kimepata mafanikio maridhawa katika ufundishaji, utafiti, huduma ya jamii na ushirikiano wa kimataifa. Mtalaa wa usimamizi wa uchumi ulipewa tuzo na kipaumbele cha ufadhili na serikali mara nyingi na mwaka 2012 mtalaa huo umekuwa kielelezo cha ufundishaji cha kitaifa. Aidha, maprofesa watano wameingia programu ya ufadhili ya wizara ya elimu kama ni wasomi mahiri.

Licha ya kuimarisha ushirikiano na vyuo vikuu vya Ulaya na Marekani, kitivo hiki kimeanzisha uhusiano na vyuo vikuu vya nchi zinazoibuka kiuchumi. Kinawahamasisha wanafunzi waende nchi za nje kusoma au kufanya vitendo. Hali kadhalika, kinadumisha ushirikiano mwema na serikali, makampuni, asasi za fedha na mashirika mbali mbali ya kimataifa.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC