CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Uhusiano wa Kimataifa

Kitivo cha Uhusiano wa Kimataifa kilianzishwa mwaka 2006 na waziri mstaafu wa mambo ya nje Bw. Li Zhaoxing ni mkuu wa heshima wa kitivo hiki. Chini ya kitivo kuna Idara ya Diplomasia, Idara ya Siasa ya Kimataifa, Idara ya Siasa na Utawala, Taasisi ya Masuala ya Kimataifa, Ofisi ya Uhariri wa Jarida“Kongamano la Masuala ya Kimataifa”, Kituo cha Utafiti wa Jinsia na Masuala ya Kimataifa, Kituo cha Uhusiano wa Mashariki na Magharibi, Kituo cha Utafiti wa Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa na Kituo cha Utafiti wa Diplomasia ya Umma.

Hadi sasa kuna walimu 25 wakiwemo maprofesa 5, maprofesa washiriki 12. 80% ya walimu wamepata shahada ya uzamivu. Isitoshe, kitivo pia kinawaalika wataalamu wa nje, maprofesa na mabalozi mashuhuri kusomesha au kuandaa mihadhara kwetu.

Kila mwaka kitivo kinasajili wanafunzi 96 na wanafunzi wageni 15-20 wa shahada ya kwanza. Programu ya M.A inadahili wanafunzi  40-45 na wanafunzi wageni 15-20 katika fani sita zifuatazo: Mifumo ya Kisiasa ya China na Nchi za Nje, Uhusiano wa Kimataifa, Siasa ya Kimataifa, Diplomasia, Utafiti wa Kanda na Diplomasia ya Umma. Na programu ya Ph.D ya Uhusiano wa Kimataifa na Utafiti wa Kanda inasajili wanafunzi 4-6 kila mwaka.

Kitivo kinatilia maanani kuinua uwezo wa lugha wa wanafunzi. 2/3 za masomo yanasomeshwa kwa Kiingereza au lugha mbili za Kiingereza na Kichina. Wakati wanafunzi wageni wa programu ya M.A wanasomeshwa kwa Kiingereza kitupu.

Kitivo hiki kimejenga ushirikiano mwema na vyuo kumi na kitu vya nje. Mathalani, kinashirikiana na Chuo Kikuu cha Hawaii katika programu ya “3+2”; kinashirikiana na Chuo Kikuu cha Denver, Chuo Kikuu cha Lancaster na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Wananchi cha Urusi katika programu ya M.A ya pande mbili; kinashirikiana na Chuo Kikuu cha Siasa cha Taiwan, Chuo Kikuu cha Chung Cheng na Chuo Kikuu cha Ualimu cha Taiwan kupelekeana wanafunzi wa muda mfupi. Kila mwaka walimu wanakwenda nchi za nje kusoma, kutembea ama kuhudhuria makongamano ya kimataifa huku wasomi wengi mashuhuri wanakuja kufanya matembezi katika kitivo hiki.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC