CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani

Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani kiliasisiwa mwaka 1994 na asili yake ilikuwa kitengo cha mafunzo ya wakalimani wa Umoja wa Mataifa kilichozinduliwa mwaka 1979. Kitivo hiki kimejenga sifa bora kwa kutayarisha wakalimani mahiri zaidi ya 700 kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mengineyo humu nchini. Kitivo kimeuandalia Umoja wa Mataifa mitihani ya Kichina mara nyingi na kutoa mafunzo mahususi kwa wakalimani kutoka Hong Kong, Macau, Singapore, programu ya China ya WTO, Benki ya Kilimo ya China, Kampuni ya Mafuta ya Petroli ya China, mkoa wa Guangxi n.k.

Hivi sasa kuna walimu 22 na maprofesa 5 kutoka nje. Walimu wote wana uzoefu mkubwa wa kutafsiri katika mashirika mbali mbali ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani na mikutano ya kimataifa.

Kuna programu ya M.A. katika Ukalimani Andamizi wa Kiingereza; Ukalimani Andamizi wa Kiingereza na lugha nyingine kati ya Kijerumani, Kirusi, Kifaransa, Kihispania, Kikorea na Kithai; Tafsiri na Ukalimani. Programu ya Ph.D inadahili wanafunzi wa mtalaa wa tafsiri na ukalimani na mtalaa wa isimu. Hadi sasa wapo wanafunzi kiasi cha 220. Wanafunzi wanaweza kufanya mazoezi katika asasi mbali mbali. Baada ya kuhitimu, wengi wao wanapata ajira katika wizara na idara za serikali, vitengo vya mambo ya nje vya mikoani, makampuni ya kimataifa na vyuo vikuu.

Kitivo hiki kimejiunga na Shirikisho la Taasisi za Tafsiri na Ukalimani Duniani (CIUTI) na pia kimeteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa kituo cha mafunzo ya wakalimani.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC