CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Sheria

Kitivo cha Sheria kiliasisiwa mwaka 2001 kama idara na kikawa kitivo cha sasa mwaka 2006. Hivi sasa kuna walimu 35 na miongoni mwao 33 wameshapata shahada ya uzamivu. Idadi ya wanafunzi imefikia 333 ikiwa ni pamoja na 228 wa shahada ya kwanza na 105 wa shahada ya pili. Programu ya M.L inadahili wanafunzi wa vipengele vitano: Sheria ya Biashara ya Kimataifa, Sheria ya Kimataifa, Sheria ya Hakimiliki, Sheria ya Makosa ya Madai na Biashara, Utekelezaji wa Sheria na Ushirikiano wa Kimataifa. Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CPPCC Prof. Luo Haocai ni mkuu wa heshima wa kitivo hiki na Naibu Spika wa Bunge la Umma Jaji Wan Exiang anasimamia taaluma za kitivo hiki kama ni profesa mkuu.

Mfumo wa masomo unaainishwa katika vikundi vinne: Sheria za China, Sheria za Uingereza, Lugha na Utamaduni wa Uingereza na Marekani, Biashara. Wanafunzi wanapohitimu wangekuwa na uelewa mzuri wa sheria za kichina na kijadi na uwezo wa utendaji wa sheria ya biashara.

Kitivo hiki kinadumisha ushirikiano wa karibu na mpana na washirika wa vyuo vikuu mbalimbali duniani kama vile Columbia, New York, Cornell, Georgetown, Pennsylvania, Oxford Brookes, LSE, Queensland, Melbourne, New South Wales, Bond, Toledo ambao ushirikiano huo umenufaisha walimu na wanafunzi.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC