CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Idara ya Kijerumani

发布时间:2019-04-28

Idara ya Kijerumani iliasisiwa mwaka 1950 ambapo kulikuwa na walimu wawili na wanafunzi 14 tu. Mwaka 2002 mtalaa huu wa Kijerumani ulipandishwa hadhi kuwa ya kitaifa.

Idara hii imeboresha mfumo wa masomo ambao unagawika katika pande sita: Fasihi, Isimu, Tafsiri na Ukalimani, Utamaduni, Diplomasia na Uchumi wa Ujerumani, Mbinu za Ufundishaji. Na wanafunzi wa mwaka wa tatu na wa nne wanaweza kuchagua kati hayo kama watakavyo.

Hadi sasa idara hii ina walimu 37 ikiwa ni pamoja na maprofesa 8, maprofesa washiriki 11 na walimu wazamivu 29. Kuna wanafunzi 345 wa shahada ya kwanza, wanafunzi 92 wa shahada ya pili na wanafunzi 25 wa shahada ya juu.

Idara hii imeanzisha ushirikiano na Chuo Kikuu cha Heidelberg, Chuo Kikuu cha Gottingen, Chuo Kikuu cha Jena, Chuo Kikuu cha Passau, Taasisi ya Ukalimani ya Munich, Chuo Kikuu cha Vienna n.k. ambapo kila mwaka walimu na wanafunzi wanapelekwa hapo kusoma. Aidha, idara hii pia imezindua programu ya M.A ya “Utafiti wa Kijerumani” tangu mwaka 2008 ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Nanjing na Chuo Kikuu cha Göttingen. Vile vile idara hii inashirikiana na Taasisi ya Kijerumani ya Taifa (IDS) na Chuo Kikuu cha Mannheim katika programu ya Ph.D.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC