CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Kiarabu

发布时间:2019-04-28

Kitivo cha Kiarabu kimepandishwa hadhi tangu Juni, mwaka 2015 kutoka idara iliyoanzishwa mwaka 1958.  Kitivo hiki kilitangulia katika China kuzindua programu za M.A na Ph.D kwa nyakati tofauti za mwaka 1981 na 1986.

Katika miaka 50 na ushei baada ya kuasisiwa, kitivo hiki kimepata mafanikio makubwa katika ufundishaji na utafiti kutokana na juhudi za walimu wetu mashuhuri wakiwakilishwa na Prof. Na Zhong na Prof. Yu Zhangrong. Hadi sasa, kuna walimu na wafanyakazi 17 wakiwemo maprofesa wanne, maprofesa washiriki wanne na walimu wanane wazamivu. Mtaalamu wa sasa Prof. Firas Sawah ni mwanazuoni mashuhuri anayejulikana kote Uarabuni.

Katika nusu karne iliyopita, kitivo hiki kimetayarisha wanafunzi zaidi ya 2,000 wanaoelimika kikamilifu katika lugha, ujuzi na tabia. Katika Wizara ya Mambo ya Nje, takriban nusu ya wafanyakazi wa Kiarabu walihitimu kutoka kitivo hicho wakiwemo Naibu Waziri Mkuu Bw. Zhang Ming na mabalozi 30 na zaidi na makumi ya mabalozi wadogo.

Muda wote lugha, fasihi na utamaduni wa Kiarabu ndio fani ya kushughulikiwa zaidi katika kitivo hiki. Ili kupanua wigo wa utafiti na kuendana na mkakati wa kitaifa, hivi karibuni kitivo hiki kimeanzisha taasisi tatu mpya, yaani: Taasisi ya Utamaduni wa Kiarabu na Uislamu, Taasisi ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari vya China na Uarabu na Taasisi ya Utafiti wa Kanda ya Mashariki ya Kati.

Kwa upande wa ushirikiano wa kimataifa, kitivo hiki kimejenga ushirikiano wa karibu na vyuo vikuu zaidi ya kumi Uarabuni ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Lebanese, Chuo Kikuu cha Ain Shams cha Misri, Chuo Kikuu cha Mfereji wa Suez, Chuo Kikuu cha Hassan II cha Morocco, Chuo Kikuu cha Pili cha Algeria, Chuo Kikuu cha Umoja wa Falme za Kiarabu, Chuo Kikuu cha Zayed cha U.A.E. n.k. Kila mwaka kitivo hiki kinawapeleka walimu na wanafunzi kusoma katika vyuo vilivyotajwa hapo juu na vingine vya Marekani, Uingereza na Israel.

Hivi leo Kitivo cha Kiarabu kimekuwa kitovu cha ufundishaji na utafiti wa Kiarabu na daraja la kukuza urafiki kati ya wananchi wa China na Waarabu.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC