Tarehe 31 Machi, Rais wa Chuo Kikuu cha Queensland cha Australia Bi. Deborah Terry ameongoza ujumbe kutembelea Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amekutana na Bi. Deborah Terry na msafara wake. Pande hizo mbili zimetiliana saini "Mkataba wa Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na Chuo Kikuu cha Queensland".