CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Toleo la Kiingereza la "Ukonfusia wa Kimataifa" Lazinduliwa katika BFSU

发布时间:2022-09-16

Tarehe 26 Agostitoleo la kwanza la Kiingereza la Ukonfusia wa Kimataifalililoandaliwa na Shirikisho la Ukonfusia wa Kimataifa(ICA) na Shirika la Uchapishaji wa Ufundishaji na Utafiti wa Lugha za Kigeni (FLTRP) limezinduliwa katika BFSU. Mkuu wa ICA Bi. Liu Yandong ametoa pongezi kwa tukio hilo.

Makamu Mkuu wa ICA Bw. Chen Lai, Katibu Mkuu wa ICA Bw. Jia Deyong, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na viongozi wengine wamehudhuria mkutano huo.

"Ukonfusia wa Kimataifa" ni jarida muhimu la ICA, pia ni daraja muhimu la kukuza mazungumzo kati ya staarabu duniani, kuongoza uvumbuzi wa kitaaluma, kuonyesha matokeo bora ya utafiti na kujenga uhusiano kati ya watu wanaotoka nchi tofauti. Shirikisho la Ukonfusia wa Kimataifa limetoa toleo la Kichina mnamo Mei 2021. Toleo la Kiingereza linakuza zaidi uenezaji na uendelezaji wa Ukonfusia wa Kimataifa na utamaduni wa jadi wa Kichina, na kuweka jukwaa kwa wataalamu na wasomi wanaoshughulikia fani hiyo ili wawasiliane kwa ufanisi zaidi.


No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC