CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

“Darasa la ukonfusia wa kimataifa na walimu wa utamaduni wa kichina la mwaka 2021”Lafunguka

Sherehe ya ufunguzi wa“Darasa la ukonfusia wa kimataifa na walimu wa utamaduni wa kichina la mwaka 2021”lililofadhiliwa na Shirikisho la Ukonfusia wa Kimataifa(ICA) pamoja na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing(BFSU) ilifanyika mnamo tarehe 20 Julai mwaka huu. Katibu mkuu wa ICA Jia Deyong na makamu mkuu wa BFSU Zhao Gang walihudhuria sherehe hiyo.

Darasa hilo la siku 13 litasomeshwa kwa Kichina pamoja na Kiingereza kwenye mtandao. Zaidi ya wanafunzi 120 wanaotoka nchi 26 wamejiunga na darasa hilo linalojumuisha walimu wa China na walimu wa nchi za kigeni. Wataalamu na wanafunzi wanaotoka karibu vyuo vikuu 50 vya ndani na nje ya nchi walishiriki kwenye sherehe hiyo ya ufunguzi.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC