CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kikao cha Ukuaji wa Lugha za Kiafrika Chafanyika BFSU

Mnamo Julai 5, kikao cha ukuaji wa kozi za lugha za kiafrika kimefanya hapa chuoni na wanadiplomasia 15 kutoka nchi 8 za Afrika wakiwemo mabalozi wa Madagaska na Somalia wameshiriki katika kikao hicho.


AD7A

Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amewakaribisha wageni waalikwa na kuongeza kuwa, lugha ni chombo cha mawasiliano na daraja la urafiki kati ya China na Afrika. Kikao hiki kimeandaliwa kwa ajili ya kukuza maendeleo ya kozi za lugha za kiafrika zinazosomeshwa katika chuo hiki na kuimarisha ushirikiano na balozi na vyuo vikuu vya nchi za Afrika katika fani ya kupelekeana walimu na wanafunzi, kuchapisha vitabu na kamusi, kufanya uchunguzi wa pamoja n.k.


Wajumbe wote waliotoka Madagaska, Somalia, Botswana, Comoro, Ethiopia, Tanzania, Zimbabwe, Morocco wametoa hotuba fupi wakisema kuwa, wamefurahia nia na juhudi za Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU) za kusomesha na kueneza lugha zao nchini China. Wameahidi kuiunga mkono BFSU kufanikisha mkakakti wa lugha za Kiafrika.


B4B5

Makamu mkuu wa chuo Prof. Jia Wenjian, Mkurugenzi wa Kitivo cha Masomo ya Afrika Prof. Li Hongfeng na walimu wa Kiswahili, Kihausa, Kizulu, Kiamhara, Kimalagasy na Kisomali wamehudhuria kikao hiki.No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC