CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Kiingereza cha Malengo Mahususi

发布时间:2019-04-28

Kitivo cha Kiingereza cha Malengo Mahususi kilichoasisiwa mwaka 2008 kinawatolea wanafunzi wa shahada zote masomo mbali mbali ya Kiingereza huku kikifanya uchunguzi wa ufundishaji wa Kiingereza cha malengo mahususi. Kuanzia Septemba, mwaka 2016 kitivo hiki kimezindua programu ya shahada ya uzamili ya tafsiri.

Licha ya masomo ya lugha, kitivo hiki kimeweka masomo yenye fani nne: Mawasiliano ya Tamaduni Mtambuko,  Kiingereza cha Malengo Mahususi, Lugha na Tafsiri, Fasihi na Utamaduni.

Hivi sasa kitivo hiki kina walimu na wafanyakazi 52 wakiwemo maprofesa 3, maprofesa washiriki 15 na walimu wazamivu 15.

Kitivo hiki kimejenga ushirikiano na Chuo cha Skagit Valley cha Washiton D.C na kupelekeana walimu kila mwaka. Sasa kitivo kinawasiliana na Chuo Kikuu cha Kansas na Chuo Kikuu cha Cambridge ili kiweze kushirikiana navyo katika siku za mbele.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC