CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Idara ya Kifaransa

发布时间:2019-04-28

Idara ya Kifaransa iliyoasisiwa mwaka 1950 inatoa programu zote za shahada za kwanza, uzamili na uzamivu ikiwa ni pamoja na MTI ya Kifaransa.

“Jifunze Kifaransa” linalochapishwa tangu mwaka 1980 ni jarida la kwanza la taaluma hiyo nchini China. Pamoja na hilo, idara hiyo imezindua jarida la “Uchunguzi wa Nchi na Kanda ya Kifaransa” tangu mwaka 2015. Aidha, idara hiyo ina Kituo cha Utafiti wa Nchi na Kanda ya Kifaransa, Kituo cha Utafiti wa Uswisi, Kituo cha Utafiti wa Ubelgiji na Kituo cha Utafiti wa Quebec.

Mpaka sasa idara hii ina walimu 24 wakiwemo maprofesa 5, maprofesa washiriki 8 na walimu wazamivu 15 ambao wamebobea katika isimu, fasihi, tafsiri na ukalimani na utafiti wa kanda na nchi. Aidha, kila mwaka inaalika wataalamu wawili kutoka Ufaransa na mtaalamu mmoja wa Ubelgiji kujiunga na kazi ya ufundishaji ya idara hiyo.

Miaka yote idara ya Kifaransa inaupa kipaumbele ufundishaji wa lugha huku ikizingatia uwezo wa wanafunzi wa kusoma, kusikiliza, kuzungumza, kuandika na kutafsiri. Kwa kufuatia uboreshaji na ukamilishaji wa masomo, wanafunzi wetu huibuka kidedea katika mitihani ya kitaifa na mashindano mbali mbali.

Idara hiyo imeingia mikataba ya ushirikiano na taasisi na vyuo vikuu 17 mathalani Taasisi ya Siasa ya Paris,  Chuo Kikuu cha Tatu cha Paris, Chuo Kikuu cha Nne cha Paris, Chuo Kikuu cha Montreal (Quebec), Chuo Kikuu cha Laval, Chuo Kikuu cha Uhuru cha Brussels, Chuo Kikuu cha Geneva n.k. Kila mwaka, wanafunzi wapatao 30-40 wana fursa ya kusomea vyuo hivyo.

Wanafunzi wa idara hiyo wana nafasi kubwa katika soko la ajira wakisifika sana kwa ustadi wa lugha na sifa bora za kiakili na kimwili. Aghalabu wanafunzi wetu huajiriwa katika vitengo vya kushughulikia mambo ya nje kama vile Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Biashara, Wizara ya Elimu, Wizara ya Utamaduni, Wizara ya Sanyansi na Teknolojia; vyombo vya habari mbali mbali kama Shirika la Habari la Xinhua, Kituo cha Televisheni cha CCTV, Redio China Kimataifa; Vyuo Vikuu na taasisi za utafiti; idara za mikoani za kushughulikia mambo ya nje; mashirika na makampuni yenye ushirikiano na nchi za Kifaransa.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC