CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

Kitivo cha Kirusi

发布时间:2019-04-28

Kitivo cha Kirusi kiliasisiwa mwaka 1941 sambamba na kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha BFSU.

Kitivo hiki kimeweka programu za shahada zote. Hadi Septemba, 2015 kuna wanafunzi 284 wa B.A, wanafunzi 46 wa M.A, wanafunzi 21 wa Ph.D, watafiti 6 baada ya Ph.D na wanafunzi watano kutoka nchi za nje. Walimu waliopo ni 23 wakiwemo maprofesa wanane (watano ni washauri wa programu ya Ph.D), maprofesa washiriki wanane na mtaalamu mmoja. Kati yao, walimu 16 wameshapata shahada ya Ph.D na walimu 5 walitunukiwa “Tuzo ya Pushkin” ambayo ni tuzo ya juu ya Kirusi duniani. Isitoshe, walimu kadhaa walipata “Tuzo ya Rais”, “Tuzo ya Urafiki”, “Tuzo ya Fasihi ya Gorky” n.k. Vitabu vya Kirusi walivyotunga vilituzwa na serikali na vinatumiwa katika vyuo zaidi ya 100 nchini China.

Kitivo hiki kinachunguza mitalaa ifuatayo: isimu, fasihi, tafsiri na ukalimani, utamaduni, utafiti wa kanda, uhusiano wa kimataifa, siasa ya kimataifa, uchumi wa Urusi. Kitivo kimeweka kozi za  kila aina katika shahada ya kwanza ikiwa ni pamoja na: Sarufi, Usikilizaji, Usomaji, Tafsiri, Ukalimani, Uandishi; Jiografia, Historia, Utamaduni, Fasihi, Jamii, Utafiti wa Kanda, Uchumi na Biashara, Diplomasia n.k. Programu ya M.A ina aina mbili. Wanafunzi wa M.A (kwa tasnifu) na Ph.D wanaweza kujiunga na programu za Kirusi cha Kisasa, Fasihi ya Kirusi, Utamaduni na Jamii na Utafiti wa Kanda.

Miaka yote kitivo hiki kinashika hatamu katika mitihani ya kitaifa na mashindano ya lugha ya namna kwa namna. Wanafunzi wanaonesha ustadi mkubwa wa lugha na uelewa mpana wa maarifa. Hivyo wanapata ajira kirahisi mwaka hadi mwaka ikiendana na ukuaji wa ushirikiano imara kati ya China na Urusi. Miaka ya karibuni, wanafunzi wanaajiriwa na wizara, idara za serikali, mashirika ya umma, makampuni ya Urusi n.k.

Kitivo hiki kimejenga ushirikiano na Chuo Kikuu cha Moscow, Chuo Kikuu cha Lugha cha Moscow, Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa ya Moscow, Taasisi ya Lugha ya Pushkin, Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi, Chuo Kikuu cha Saint Petersburg. Kila mwaka kitivo kinawapeleka walimu na wanafunzi kusoma katika vyuo hivyo. Halikadhalika wanafunzi wa nje wanakaribishwa kusoma Kirusi katika kitivo hiki.

Katika kipindi kipya cha mageuzi ya elimu, kitivo hiki kimeweka malengo ya kuandaa mahiri wa hali ya juu kwa kupitia mbinu bora za ufundishaji na raslimali nyingi za utafiti ili kukidhi mahitaji ya jamii katika fani za tafsiri na ukalimani, utafiti wa kanda na usambazaji wa utamaduni wa kichina na wa kirusi.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC