CHUO KIKUU CHA LUGHA

ZA KIGENI, BEIJING

BFSU yaandaa Jukwaa la Maendeleo ya Tibet ya China la 2023

发布时间:2023-05-29

Mnamo tarehe 23 Mei, “Jukwaa la Maendeleo ya Tibet ya China la 2023” limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Beijing. Kaulimbiu ya jukwaa hilo ni "Zama Mpya, Tibet Mpya na Safari Mpya". Jukwaa hilo limeandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, Serikali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet pamoja na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na walimu wengi wa kigeni wamehudhuria jukwaa hilo. Mabalozi, wakuu wa vyombo vya habari vya kigeni nchini China, wataalamu, wanafunzi wanaotoka nchi na maeneo 36 wameshiriki katika jukwaa hilo.

Prof. Yang Dan ametoa hotuba kwenye kongamano kuu akieleza mafanikio yaliyopatikana ya kiuchumi ya Tibet. Kwa kuzingatia hali ya kiuchumi na kijiografia katika Tibet, ametoa mashauri kwa maendeleo ya ustawi wa pamoja ya Tibet.

Jukwaa hilo limekuwa na vikao sambamba vitano, na kikao cha "Maendeleo yenye Ubora wa Juu na Ustawi wa Pamoja katika Tibet" kimeandaliwa na BFSU.


No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

OFFICE FOR INTERNATIONAL EXCHANGE AND COOPERATION

OFFICE OF CONFUCIUS INSTITUTES

OFFICE FOR OVERSEAS STUDENTS AFFAIRS

GENERAL ADMINISTRATION OFFICE

Copyright@BFSU.Support by ITC