Utangulizi

Mfumo na Semesta

Elimu ya Digrii

Uombaji na Udahili

Kuhusu Malazi

Ada za Shule

Mfumo na Semesta

Mwaka wa masomo wa BFSU unagawanyika katika mihula miwili – muhula wa Fall (mwanzoni mwa Septemba – katikati ya Januari) na muhula wa Spring (mwishoni mwa Februari – katikati ya Julai). Kila mwaka mwanafunzi huwa anapata mapumziko mara mbili – likizo ya siku za joto (Julai na Agosti) na likizo ya siku za baridi (wiki 4 hivi ikiwa ni pamoja na Sikukuu ya Spring ya China). Kozi fupi ya Kichina hutolewa katika likizo.

Elimu ya Digrii

1. Programu ya shahada ya kwanza huendeshwa kwa miaka minne. Wanafunzi wakishamaliza kozi zote na kufaulu kwenye utetezi wa tasnifu ndipo wanatunukiwa cheti cha kuhitimu masomo na shahada ya kwanza

2.Programu ya shahada ya uzamili huendeshwa kwa miaka 2 au 3 ikitegemea programu yenyewe. Wanafunzi wakishatimiza alama zinazotakiwa na kufaulu kwenye utetezi wa tasnifu ndipo wanatunukiwa cheti cha kuhitimu masomo na shahada ya uzamili.

3.Programu ya shahada ya uzamivu huendeshwa kwa miaka 3. Wanafunzi wakishatimiza alama zinazotakiwa, kuchapisha kazi za utafiti na kufaulu kwenye utetezi wa tasnifu ndipo wanatunukiwa cheti cha kuhitimu masomo na shahada ya uzamivu.

Elimu ya Cheti

1.Kozi za Kawaida: Wanafunzi wanaweza kusoma Kichina ama kozi nyingine kwa muda wa nusu mwaka hadi mwaka mzima, ingawaje muda huo unaweza kuongezeka iwapo kuna sababu ya kufanya hivyo. Wakishafaulu kwenye mtihani ndipo wanapewa cheti husika.

2.Kozi ya Muda: Kwa sasa kuna kozi ya Kichina tu ambayo inaendelea kwa wiki 3, wiki 4 na wiki 8 katika siku za joto ama kozi ya wiki 4 katika siku za baridi. Darasa linaanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Asubuhi ni lugha ya Kichina na mchana ni utamaduni wa kichina. Aidha, wanafunzi wanapangiwa matembezi ya mjini Beijing kila wiki. Wanafunzi watapewa cheti wakishamaliza masomo.

Uombaji na Udahili

 

1.Uombaji:Wanafunzi wanaweza kuwasilisha maombi yao pamoja na pasipoti na cheti husika kupitia tovuti yetu (http://study.bfsu.edu.cn). Muwasilishe maombi kati ya katikati ya Aprili hadi mwanzoni mwa Juni kwa ajili ya muhula wa Fall, ama kuanzia katikati mwa Oktoba hadi mapema mwa Januari kwa muhula wa Spring. Tutapitia nyaraka zote na kuandaa mtihani utakapohitajika. Mufuatilie maendeleo ya usajili kwa kupitia tovuti yetu.

2Udahili: Endapo utakuwa umedahiliwa, tutakutumia barua ya udahili, fomu ya maombi ya visa (JW202) na barua ya ukaribisho mapema kadiri iwezekanavyo. Mchakato huo utachukua wiki 4-5.

 

Kuhusu Malazi

Chuo kikuu kinatoa huduma za mabweni ya aina tofauti kwa wanafunzi wageni. Kama hupendi kuishi chuoni, basi utapaswa kujitafutia makaazi mwenyewe mapema na kuripoti kwenye kituo cha polisi kilicho karibu ili upewe thibitisho la makaazi ambalo litahitajika wakati wa kujiandikisha BFSU na kuomba visa.

Ada za Shule

Programu

Ngazi ya Elimu

Kiasi cha Ada

Ada ya Usajili

Degree programs      
Kichina Shahada ya Kwanza 12,150 RMB / Muhula

22,150 RMB / Mwaka

400 RMB
  Shahada ya Uzamili 27,000 RMB / Mwaka 800 RMB
Nyingine Shahada ya Kwanza 26,000 RMB / Mwaka 800 RMB
  Shahada ya Uzamili 27,150 RMB / Mwaka 800 RMB
  Shahada ya Uzamili ya Tafsiri na Ukalimani 30,000 RMB / Mwaka 800 RMB
  Shahada ya Uzamivu 34,000 RMB / Mwaka 800 RMB
Elimu ya Cheti      
Kichina Kozi ya Kawaida 11,150 RMB / Muhula

21,150 RMB / Mwaka

400 RMB

welcome to our bfsu

online registration

it doesn't take a genius to start and also can become the best person

click here

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

Office for International Exchange and Cooperation

0086-10-88816715
[email protected] https://international.bfsu.edu.cn/en/
General Administration Office

0086-10-88816215
[email protected]