Waziri Mkuu wa Uholanzi Azuru BFSU

April 12 mchana, Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amefanya ziara katika chuo chetu akiambatana na balozi wake nchini China, katibu mkuu wa Ofisi ya Waziri mkuu, mshauri wa sera ya mambo ya nje na ulinzi na mkurugenzi wa Idara ya Asia n.k.

Mkuu wa Chuo Prof. Peng Long ameandaa sherehe ya kumkaribisha Bw. Rutte akimshukuru mgeni huyu kutenga muda maalum kuizuru BFSU. Katika hotuba yake, Prof. Peng amewaelezea wageni hali ya kozi ya Kidachi akisisitiza kuwa kozi hiyo si kituo muhimu cha kuandaa wasomi wa lugha tu, bali pia ni jukwaa la kutafiti na kueneza utamaduni wa Uholanzi.

Bw. Mark Rutte amefurahia juhudi za chuo chetu kukuza lugha na utamaduni wa nchi yake baada ya kuzungumza na wanafunzi wa Kidachi kuhusu maswali mbalimbali. Bw. Rutte ameridhika sana na ziara hiyo yenye manufaa. Kuhusu ushirikiano wa elimu kati ya nchi mbili, Bwana huyo amesema elimu zote zinadhamiria kusaka ujuzi uliopo na kuvumbua ujuzi mpya ingawa mifumo yake ipo kwenye aina tofauti.

Kabla ya sherehe hiyo, Bw. Rutte amezunguka chuo kizima ikiwemo bustani ya urafiki wa China na Ulaya kwa kupanda baiskeli. Balozi wa China nchini Uholanzi Bw. Wu Ken amehudhuria sherehe hiyo ambayo iliendeshwa na makamu mkuu wa chuo Bw. Yan Guohua.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

Office for International Exchange and Cooperation

0086-10-88816715
[email protected] https://international.bfsu.edu.cn/en/
General Administration Office

0086-10-88816215
[email protected]