Peng Long Ahutubia Mkutano wa Taasisi za Confucius za Dunia

Mkutano wa 12 wa Taasisi za Confucius za Dunia ukiwa na kaulimbiu ya “Kushirikiana na Kuendelea kwa ubunifu ili kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja” umefunguliwa mjini Xi’An tarehe 12, Disemba. Naibu Waziri Mkuu na mwenyekiti wa Baraza la Makao Makuu ya Taasisi za Confucius Bi. Liu Yandong amefungua mkutano huo na kutoa hotuba.

Mkuu wa chuo Prof. Peng Long na makamu mkuu Prof. Yan Guohua wamealikwa kuhudhuria ufunguzi wa mkutano huo. Kwa niaba ya zaidi ya taasisi nyingine 220, Prof. Peng ametoa hotuba akidhihirisha kuwa, katika zama hizi za utandawazi na teknolojia ya habari, taasisi za Confucius zina nafasi kubwa na pekee ya kuleta uelewano kati ya watu wa nchi mbalimbali.

Taasisi ya Confucius ya Sofia (CIS) inayoendeshwa na chuo chetu imetunukiwa tuzo ya “Taasisi Bora ya Confucius” huku mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Confucius ya Munich (CIM) Bw. Jakob Pöllath na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Hankuk Bw. Kim In Chul wakitunukiwa tuzo ya “Wafanyakazi Bora”. Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Malaya (KITCLUM) imepewa tuzo ya “Taasisi Bora kwa Mtihani wa HSK”.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)

Office for International Exchange and Cooperation

0086-10-88816715
[email protected] https://international.bfsu.edu.cn/en/
General Administration Office

0086-10-88816215
[email protected]