Taasisi ya Ulinganishi wa Tamaduni na Mawasiliano ya Wanadamu Yaasisiwa

%e5%8c%97%e4%ba%ac%e5%a4%96%e5%9b%bd%e8%af%ad%e5%a4%a7%e5%ad%a6%e6%af%94%e8%be%83%e6%96%87%e6%98%8e%e4%b8%8e%e4%ba%ba%e6%96%87%e4%ba%a4%e6%b5%81%e9%ab%98%e7%ad%89%e7%a0%94%e7%a9%b6%e9%99%a2%e6%88%90Tarehe 6 Desemba, Taasisi ya Ulinganishi wa Tamaduni na Mawasiliano ya Wanadamu imeasisiwa katika Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Mwenyekiti wa Shirikisho la Confucianism la Kimataifa Bw. Teng Wensheng na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Jamii ya Wizara ya Elimu Bw. Zhang Donggang wameshuhudia uzinduzi huo.

Kwa kutegemea idadi kubwa za lugha katika BFSU, taasisi hiyo inanuia kutafiti na kulinganisha masuala ya utamaduni zikiwemo historia, dini, falsafa n.k. kati ya China na nchi nyingine za dunia ili kubainisha sifa pekee za staarabu mbalimbali pamoja na nafasi ya ustaarabu wa kichina katika dunia.

Prof. Zhang Qizhi ni mkurugenzi wa heshima wa taasisi hiyo, Prof. Han Zhen ni mwenyekiti wa Kamati ya Akademia, Prof. Peng Long ni mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji na Prof. Zhang Xiping ni mkurugenzi wa taasisi hiyo.

No. 2 North Xisanhuan Road, Beijing, P.R.China. (100089)